MTANGAZAJI

MCH KENAN MWASOMOLA APATA AJALI


Mwenyekiti wa Konferensi ya Nyanda za Juu Kusini nchini Tanzania ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato  Mchungaji Kenan Mwasomola Amepata ajali  Saa 2 Usiku Juni  29,mwaka huu  eneo la Nyandekwa katikati ya Igunga na Nzega wakati akielekea Kirumba Mwanza kwa Sherehe ya Jubilee ya miaka 50 akiwa na Gari la ofisi.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Shuhuda wa Ajali hiyo ambaye pia alikuwa ndani ya Gari hilo Mch. D Bambaganya amesema Mwenyekiti huyo ameumia mbavu na mke wa Mwasomola ameumia shingo na bega na tayari wote wamelazwa Hospitali ya Mission ya Nkinga Na hali zao Zinaendelea Vizuri. 

Sababu ya Ajali inasemekana ni Tuta lililo kuwa katika barabara ambayo lami imekwanguliwa na kulikuwa hakuna alama yeyote ya kuelekeza. Jambo lililo sababisha Gari kubilingita juu chini na hatimaye kusimama. 

Kwa Mujibu wa wenyeji wa eneo hilo wanasema Tuta hilo limesha sababisha Ajali nyingi zilizo poteza maisha ya watu. Tena hata asubuhi hii wakati nikipokea habari hizi kunagari jingine dogo nusula lipate ajali.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.