AUDIO NA PICHA:TUKIO LA WANATEKNOHAMA NA WANAHABARI WAADVENTISTA WA SABATO TANZANIA (TAiN)WALIVYOKABIDHI BAISKELI KWA MLEMAVU
Mkutano wa Wadau wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kanisa la Waadventsta Wa Sabato Tanzania (TAiN) umetoa msaada wa baiskeli ya Walemavu (Wheel Chair) yenye thamani ya shilingi laki tatu pamoja na pesa taslimu shilingi 45,000 za Tanzania kwa Paulo Kigombe.
Paulo Kigombe ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano wa Kanisa la Mugaja Bunda Mara ndiye mjumbe pekee mwenye ulemavu wa miguu miongoni mwa wajumbe wapatao 200 wanaohudhuria mkutano wa TAiN2016 unaofanyika Dodoma,Japo kuwa ni mlemavu alikuwa akifika kwenye mkutano kwa wakati toka kuanza kwa mkutano huo unaotarajiwa kumalizika Julai 11.
Mch David Makoye ambaye ni Katibu Mkuu wa Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania ndiye aliyekabidhi baiskeli hiyo .
Sikiliza tukio hilo lilivyofanyika
Post a Comment