RAIS UHURU KENYATTA ASHIRIKI UZINDUZI WA JENGO LA OFISI ZA UNIONI KONFERENSI YA KANISA LA WA SABATO NCHINI KENYA
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameshiriki na viongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye uzinduzi wa ofisi za Unioni Konferensi ya Magharibi mwa Kenya.
Kwenye uzinduzi huo uliofanyika huko Kisumu ulihudhuriwa na viongozi wandamizi wa ECD wakiongozwa na Dr Blasious Ruguri ambaye ni Mwenyekiti wa eneo hilo linalojumuisha nchi 11.
Rais Kenyata amelipongeza kanisa la Waadventista Wa Sabato kwa namna linavyojishughurisha katika kutatua matatizo ya jamii hasa kwa vijana na hivyo akasisitiza kwa serikali kushirikiana na kanisa hilo katika kusogeza mbele maendeleo katika jamii ambapo alichangia sh.milioni 2 za Kenya kwa ajili ya vyombo vya habari katika Unioni Konferensi hiyo.
Post a Comment