MTANGAZAJI

UN YAIPONGEZA TANZANIA KWA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KUKABILI UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez  
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Umoja wa Mataifa umepongeza mashirika mbalimbali na serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua kukabiliana na vitendo vya kikatili vya ukeketaji.

Aidha imepongeza wito kutoka katika mashirika mbalimbali ya kutaka kuwapo na mabadiliko katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuzuia ndoa za utotoni.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam imesema kwamba kitendo cha kuwapo na ushawishi wa kutaka mabadiliko kwa sheria hiyo ya ndoa ni dalili kwamba watanzania wanataka kuona kwamba ndoa za utotoni zinamalizwa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu amesema katika taarifa hiyo kwamba kitendo cha saini kuendelea kuchukuliwa wakati wa siku ya kimataifa ya kupiga vita ukeketaji Februari 6 mwaka huu kunaonesha kwamba watanzania wako tayari kuzuia ndoa za utotoni.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2010, asilimia 15 ya watanzania wamekeketwa, huku wengi wakiwa mkoa wa Manyara asilimia 77.

Kwa mujibu wa Azimio la Beijing dunia ilikubaliana kwamba mtoto wa kike asilazimishwe kuolewa na pia umri wa kuolewa unapaswa kuwa miaka 18.

Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtoto wa miaka 15 anaweza kuolewa huku akiwa na miaka 14 mahakama inaweza kuridhia ndoa.

Taarifa ya Umoja huo imesema kwamba Tanzania pamoja na nchi nyingine ubaguzi kwa mwanamke unaendelea kupitia sheria na tamaduni mbalimbali huku imani za kidini zikiimarisha ubaguzi huo.

wanawake

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.