Magreth - mama anayejitambua kama Nabii, ametokea akidai ana ujumbe
aliopewa na Mungu kuwaonya wanawake (hasa wakristo) wasivae nguo
zinazoonesha maungo yao bali wavae nguo kama hiyo aliyovaa yeye (pichani
kulia).
Nilikutana na Magreth alipokuja kwenye semina ya uongozi
iliyokuwa inahitimishwa leo hapa Mwenge ili aonane na viongozi wa
Konferensi na Union awaambie kile Mungu alichomwagiza kwao.
Hapa
anajaribu kujibu maswali kutoka kwa Ndugu Mduma.
Magreth ni Mwaadventista anayesali katika kanisa la
Kipunguni Ukonga,jijini Dar es salaam na anaonekana kukiamini kwa dhati (conviction)
hicho anachokiita mafunuo.
|
Post a Comment