LUDEWA:WANANCHI WA KIJIJI CHA AMANI WAILALAMIKIA KAMATI YA AFYA YA KIJIJI CHA AMANI
Wananchi wa Kijiji cha Amani Katika Kata ya Mundindi wilayani Ludewa Mkoani Njombe wameilalamikia Kamati ya Afya ya kijiji hicho kwa kosa la kuto fuatilia dawa katika zahanati hiyo hali inayo wagharimu wananchi hao kuwapeleka wagonjwa katika hospitali ya Lugarawa.
Wanachi hao wamedai kuwa waganga wa hospitali hiyo kwa kuto wajali wanapofika katika kituo hicho na muda mwingine waganga hao kutoa kauli za kwamba wao wapo likizo badala yake wawatafute waganga wa mtaani.
Blog hii imefika katika kituo cha Afya cha zahanati ya Amani ili kuwapata waganga hao japo wazungumzie changamoto hiyo lakini Waandishi wa Habari wamewakosa waganga hao.
Post a Comment