DAR ES SALAAM:JESHI LA POLISI NCHINI TANZANIA LAWASHIKILIA MAOFISA 12 WA TRA
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Tanzania - CP, Diwani Athuman |
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai- CP, Diwani Athuman amewataja watuhumiwa watano wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Tiagi Masamaki, ambaye ni Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Habib Mponezia, ambaye ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Ushuru na Eliachi Herieli Mrema, Msimamizi Mkuu wa ICD - Azam.
Wengine ni Haroun Mpande wa Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT - TRA na Khamis Ally Omary ambaye ni Mchambuzi Mwandamizi wa masuala ya Biashara TRA.
Hata hivyo mkurugenzi huyo wa makosa ya Jinai hakuwataja watuhumiwa wengine saba wanaoshikiliwa na jeshi hilo kutokana na sababu za upelelezi, ambapo alisema wanatarajia kukamilisha uchunguzi mapema iwezekanavyo na kuwafikisha mahakamani mara moja.
Novemba 27 mwaka huu, Waziri Mkuu bwana Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kikazi ya kushtukiza katika bandari ya Dar Es Salaam ambapo aliibua kashfa hiyo ya wizi wa makontena na ukwepaji wa kodi wa takribani shilingi za kitanzania bilioni 80.
Sikiliza taarifa ya VOA hapa kuhusu taarifa ya Jeshi la Polisi
Post a Comment