DAR ES SALAAM:SERIKALI YAIPONGEZA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA TAASISI YA DORIS MOLLEL FOUNDATION ZA KUSAIDIA WATOTO NJITI!
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akizungumza mbele ya
wanahabari, madaktari na baadhi ya akina mama waliokuwa na watoto
waliozaliwa kabla ya wakati maarufu kama Njiti (Hawapo pichani). Kushoto
ni DoriS Mollel ambaye ni Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Doris Mollel Foundation (DMF) na wengine ni maafisa kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza
juhudi binafsi zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF)
katika harakati zake za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati
(njiti) na mambo ya elimu hapa nchini huku ikiahidi kuendelea
kushirikiana nayo kufikia malengo yake.
Kauli
hiyo imetolewa mapema na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi
Meck Sadiki wakati wa kupokea vifaa maalum vya kusaidia watoto njiti
vilivyotolewa na taasisi hiyo ya Doris Mollel Foundation tukio
lililofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jengo la Watoto.
Mkuu
wa Mkoa huyo aliongeza kuwa, Mashirika mengine yaendelee kujitokeza
kusaidia huduma za kijamii ikiwemo vifaa kama taasisi ya Doris Mollel
kwani asilimia 100 ya wagonjwa na watu wengine wenye mahitaji katika
tiba wanakimbilia Dar es Salaam hasa Hospitali ya Muhimbili.
Hata
hivyo kwa upande wake Mwanzilishi na mtendaji Mkuu wa DMF, Doris
Mollel amemweleza Mkuu wa Mkoa Meck Sadik kuwa wataendelea kushirikiana
na Serikali bega kwa bega katika juhudi za kusaidia watoto njiti nchini
ikiwemo kutoa elimu, vifaa na usaidizi kwa jamii dhidi ya kukabiliana
na watoto njiti nchini.
Katika
tukio hilo, Mkuu wa Mkoa alishudia vifaa hivyo na kupokea kutoka DMF
sambamba na kutembelea wodi ya watoto njiti pamoja na ile ya Kangaroo
ambayo wamama wenye watoto njiti wanakuwa wanapatiwa uangalizi maalum
dhidi ya watoto wao ikiwemo kupata joto la Mama na baadae alipanda mti
maalum mbele ya jengo hilo la Watoto kama kumbukumbu na juhudi za wadau
katika kusaidia jamii dhidi ya watoto njiti.
DMF
imeweza kusaidia vifaa katika wodi hiyo ya watoto Muhimbili vikiwemo
(Suction machines, Oxygen Concentrators na Feeding tubes). Aidha Doris
Mollel amebainisha kuwa baada ya hapo wanatarajia kuelekea mikoa ya
Kanda ya Ziwa kutoa vifaa kama hivyo huku lengo ikiwa ni kufika mikoa
yote ya Tanzania.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo maalum
la taasisi ya DMF ilipotoa vifaa hivyo katika kitengo cha Jengo la
Watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik akipata maelezo juu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya DMF.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam akimpatia zawadi ambayo ni jozi ya soksi kwa
ajili ya kusaidia watoto njiti kwa mmoja wa wamama waliokuwa katika
wodi hiyo ya watoto njiti.
Keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya siku maalum ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati maarufu njiti
Mtoto Amne Salim (3) ambaye ni njiti akikata keki maalum kwa niaba ya watoto wenzake katika tukio hilo mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimlisha keki mtoto Amne Salim katika tukio hilo.
Mtoto Amne Salim akimlisha keki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik katika tukio hilo.
Baadhi
ya akina mama waliokwenye mpango maalum wa kutunza watoto wao
waliozaliwa njiti ujulikanao kama Kangaroo wakiwa wodini mapema leo
wakati wa ugeni wa DMF na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam walipotembelea
wodi hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaamm Meck Sadik akipokea na kukabidhi vifaa maalum
kwa ajili ya kusaidia watoto njiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation mapema leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik akipanda mti maalum baada ya zoezi
hilo la Taasisi ya Doris Mollel Foundation kutoa misaada ya vifaa vya
watoto njiti.
Mama mzazi wa Doris Mollel akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Post a Comment