DAR ES SALAAM:WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAWATAKA WATANZANIA KUTUMIA FURSA ZA UTALII
Adelheim James Meru |
Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania imewataka watanzania kutumia fursa za Utalii zilizopo nchini ili kunufaika kiuchumi.
Wito huo umetolewa leo Oktoba 1 jijini Dar es salaam na Viongozi wa Wizara wakati wa ufunguzi wa maonesho
ya kimataifa ya kukuza biashara ya utalii ya Swahili SITE ambapo wamesema watanzania ni bora wakatumia vyema fursa hiyo ili kukuza
pato la taifa kupitia sekta ya utalii
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii nchini humo
Adelhelm James Meru ameeleza mafanikio ya sekta ya utalii kwa asilimia 18
ambapo idadi ya watalii wanaoingia Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2014 walikuwa
si chini ya milioni moja hivyo amewataka wadau wa sekta ya utalii nchini Tanzania kuboresha vituo
vya utalii vilivyopo ili kuongeza idadi kubwa ya watalii wanaozidi kutembelea nchini humo.
Post a Comment