DAR ES SALAAM:MASHARTI MAWILI YA KUPIGA KURA WA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA NCHINI TANZANIA HAYA HAPA
![]() |
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzana (NEC) imesema waliopoteza
vitambulisho vya kupigia kura wataweza kupiga kura endapo watakuwa na taarifa
ya polisi na majina yao kuwamo
katika daftari la mpiga kura.
Kamishna wa NEC, Mary Stelalongwe ametoa ufafanuzi huo
kutokana na kuwepo kwa watu wanaozunguka mitaani kuandika namba za vitambulisho
vya wapiga kura na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kosa ingawa amesema Tume haina taarifa rasmi ya matukio hayo.
Naye Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema
tume imepeleka taa katika vituo vyote vya kupigia kura kuepuka kura kuhamishwa na kuhesabiwa sehemu nyingine hivyo
taa hizo zimesambazwa vyote vya kupigia kura ambavyo ni 72,000 nchi nzima.
Akizungumzia mchango
wa vyombo vya habari katika uchaguzi mkuu , Jaji Lubuva ameviomba viisaidie
tume kutoa taarifa sahihi ili
uchaguzi uwe wa amani na kuonya kuwa vyombo vya habari havitaruhusiwa
kutangaza mshindi wa uchaguzi kabla ya kutangazwa na mamlaka husika ingawa
wanaruhusiwa kuripoti matokeo katika
vituo kama yalivyo
Post a Comment