MWANZA:TAMASHA LA THE LIGHTBEARERS JIJINI MWANZA KUFANYIKA SEPTEMBA 5,2015
The LightBearers |
Ziara ya waimbaji wa The LightBearers toka JCB Studioz za jijini Dar es salaam inaendelea,baada ya kushiriki kwenye tamasha la aina yake lililofanyika Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita ,mwisho wa juma hili waimbaji hao watakuwa jijini Mwanza ambapo watafanya tamasha la uimbaji ukumbi wa Vijana Social uliopo Mlango Mmoja jijini humo wakishirikiana na waimbaji mbalimbali.
Tamasha hilo ambalo litafanyika Septemba 5,2015 litakuwa pia ni kwa ajili ya kutambulisha toleo lao la tatu la audio liitwalo Mungu Kimbilio
Zaky Maduhu mwimbaji wa sauti ya nne amezungumza na blog hii
Post a Comment