MTANGAZAJI

LONDON:GOD'S DIAMOND WASHIRIKI KWENYE CHANGIZO LA MIRADI YA AFRIKA

Kwa mara nyingine tena, muziki wa injili umefanya tofauti katika maisha ya watu wasio mpenda Mungu huko nchini Uingereza. 

Mwanzoni mwa juma hili huko Kent, mjini London, vijana waimbaji wa God's Diamond tokea Kanisa la Waadventista Wasabato mjini Reading,ambao wanatoka katika jamii ya Watanzania waishio nchini Uingereza,  wameonyesha tofauti katika tukio makini la uchangiaji kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa mitatu Africa ya Kusini. Miradi yenyewe ni:

1. Mathomomayo Drop In Centre
2. Morning Star Children's Centre
3. The Global White Lion Trust.

God's Diamond  katika picha ya pamoja na waandaaji , tokea kushoto kwenda kulia ni:
1. Jane Hamer (mzungu) ambaye ni mwalimu mwandamizi katika shule ya George Abbot, iliyo Guildford-Uingereza akisimamia kitengo cha
mahusiano ya kimataifa
2. Alice Champanda-Muimbaji
3. Rachel Champanda-Muimbaji
4. Vivian Shelufumo-muimbaji
5. Reverend Ingrid ambaye ndiye muandaaji wa tukio hilo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.