MTANGAZAJI

MAURITIUS:SUPERSPORT KWENDA LAIVU ALL AFRICAN GAMES


D3A_3549
Meneja Mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa Kusini mwa Afrika, Graeme Murray akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika (hawapo pichani) katika hoteli ya OutriggerHotel & Beach Resort nchini Mauritius.

SuperSport imetangaza rasmi kwamba watashika usukani wa kurusha matangazo ya michezo ya 11 ya Afrika Games kupitia SuperSport 9 Michezo hiyo imeanza juzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkusanyiko mkubwa wa MultiChoice uliohusisha waandishi wa habari, masupastaa na chaneli wanazofanya kazi nazo katika hoteli ya OutriggerHotel & Beach Resort nchini Mauritius.

Naicker alisema kwa kujiamini kwamba urushaji wa matangazo hayo ni sehemu ya uuzaji wa sura ya michezo ya Afrika katika mabara mengine.

Akiwa katika mazungumzo hayo ambayo yalioongozwa na  mmoja wa watu wanaotoa burudani kubwa ya utangazaji ndani ya SuperSport, Carol Tshabalala alisema hali hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta nzima ya burudani na michezo na kampuni ya MultiChoice.

D3A_3571
Mkuu wa masoko wa SuperSuport, Motheo Matsau akifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika visiwa vya Mauritius.

Katika mazungumzo hayo ambapo  pia alikuwapo Mkuu wa masoko wa SuperSuport, Motheo Matsau, Meneja mkuu wa SuperSport kwa ukanda wa Kusini mwa Afrika, Graeme Murray na mgeni maalum  Anthony Baffoe, mchezaji wa zamani wa kimataifa na Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Naicker alisema ubora wa chaneli yake unatokana na kuweza kunoa vipaji vya watangazaji wake kufikia kiwango cha juu kabisa cha ubora.

Kama mwekezaji mkubwa wa masuala ya michezo katika bara la Afrika, SuperSport imepata matokeo ya kuridhisha na yenye tija.


D3A_3677
Mchezaji wa zamani wa kimataifa na Mratibu mkuu wa FIFA na CAF, Anthony Baffoe akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani)

D3A_3659
Mkuu wa uzalishaji wa SuperSport, Alvin Naicker akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).


D8A_1013
 Carol Tshabalala wa Supersport akiendesha mkutano na waandishi wa habari.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.