DAR ES SALAAM:SERIKALI YATAKIWA KUFANYA MABADILIKO YA KISERA KUWEZESHA KUKUA KWA VIWANDA VIDOGO NA VYA KATI NCHINI TANZANI
Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akifungua warsha.
Mwasilishaji wa mada Hossana Mpango akizungumza na washiriki (hawapo pichani) kwenye warsha hiyo.
Washiriki wa warsha ya siku moja ya ujasiriamali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).
Serikali imetakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kisera kuwezesha kukua kwa viwanda vidogo na vya kati nchini.
Kauli
hiyo imo katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF) kuhusu ukuaji wa sekta hiyo katika muktadha wa upatikanaji
wa fedha.
Akiwasilisha
utafiti huo mmoja wa watafiti Hossana Mpango alisema kwamba kwenye
utafiti wao wamebaini mgongano mkubwa wa kisera na utendaji,
unaosababisha kukwama kwa maendeleo ya sekta hiyo.
Alisema
ingawa kuna tatizo kubwa la ajira ambalo limefanya watu wengi
kukimbilia kujiajiri wenyewe, kuna changamoto kubwa katika sekta hiyo
hasa sera na uwapo wa mlolongo wa taasisi zinazopishana mamlaka na huku
wakiwa ndio wanatoa leseni.
Alizitaja
taasisi hizo zinazopishana mamlaka kama Shirika la Viwango nchini
(TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mamlaka ya kodi (TRA)
halmashauri mbalimbali nakadhalika.
Alisema
mabadiliko ya kisera yatawezesha kutengeneza muundo unaojali ukuaji wa
sekta hiyo hasa kwa kuangalia kodi zinazolipwa ambazo kwa sasa ni za
aina moja bila kuangalia uwekezaji unaohusika.
Sekta
hiyo ya wajasirimali wadogo na wa kati yenye watu milioni 3 kwa mujibu
wa utafiti wa mwaka 2012 inakabiliwa na tatizo la kutokua kutokana na
vikwazo mbalimbali vikiwemo pia kukosekana kwa mafunzo ya ujasirimali na
uwezo wa kupata fedha za mtaji.
"Ni
dhahiri upatikanaji wa fedha kutoka nje ili kuendeleza mtaji ni tatizo.
Lakini tatizo hili linakuwagumu zaidi kutokana na riba kubwa,
uchelewefu wa kupata mikopo, rushwa katika utoaji na ukosefu wa nidhamu
ya fedha kwa wakopaji” alisema Hossana.
Alisema
pamoja na mambo hayo kuna matatizo mengine makubwa yanayokwamisha
ukuaji wa sekta hiyo. Matatizo hayo mengine ni gharama kubwa
zinaootokana na haja ya kukidhi masharti ya uendeshaji wa viwanda hivyo
vidogo na vya kati, tozo zinazojirudia, ukosefu wa soko na elimu ndogo
ya wajasirimali.
Alisema
mabadiliko ya kisera yatasaidia kuimarisha sheria na kuweka sawa
mwelekeo wa sekta hiyo kwa kuzingatia kwamba inahitaji mchango mkubwa wa
nje ili kukua.
Alisema
mathalani ingawa kuna SACCOS, taasisi hizo zinashindwa kwenda kukopa
kutokana na riba kubwa na kuwapo kwa mfumo wa kodi na makato mengine
yakiwemo ya tozo usiokuwa na tija.
Alisema
suluhu nyingine inayostahili kufanywa ni kwa taasisi za kifedha kufuata
tabia njema za kimataifa za utoaji wa mikopo unaozingatia pamoja na
mambo mengine ukubwa wa mikopo na malipo kwa kuangalia manufaa ya
kiuchumi.
"Ili
viwanda hivi vya chini na kati kukua masuala ya kifedha na yasiyo ya
kifedha ni lazima yaangaliwe na kushughulikiwa..." alisema.
Matatizo
mengine ni pamoja na sekta hiyo kukosa msaada huku taasisi mbalimbali
zinazohitaji kushirikiana zikifanya vitu kila mmoja na wake.
Taasisi hizo ni SIDO, TRA, WDF, YDF, BRELA na pia miundombinu inayokera katika maeneo hasa ya vijijini.
Pia
ili kukuza sekta hiyo ni vyema serikali ikatengeneza miundombinu
inayojikidhi haja ya ukuaji wa sekta hiyo kama maghala, masoko, barabara,
maji, umeme kwa lengo la kupunguza gharama za kufanya biashara.
Pia
utafiti huo ulishauri kwamba serikali ni lazima kutenga fungu ambalo
litatumiwa na taasisi kama SIDO, NEEC na hata maofisa biashara wa
wilaya kwa ajili ya mafunzo ya ujasirimali na uendeshaji wa biashara.
Mapema
Mkuu wa idara ya utafiti na machapisho wa ESRF Profesa Fortunata
Makene, aliwataka washiriki wa warsha hiyo kutoa michango katika
kuboresha uelewa ili serikali iweze kutatua kizungumkuti cha ukuaji wa
sekta hiyo.
Post a Comment