MARA:TAARIFA KUHUSU MKUTANO MKUU WA KONFERENSI YA MARA YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ZIKO HAPA

Mkutano Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika Konferensi ya Mara umeanza leo huku ukitarajiwa kuhitimiswa Septemba 22
mwaka huu,ambapo unawakutanisha wajumbe zaidi ya mia tano kutoka makanisa yote ya jimbo
hilo.
Jimbo la Mara ni moja kati ya majimbo manne
yanayounda Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania, majimbo mengine yakiwa ni jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Tanzania, jimbo la Nyanza Kusini na jimbo la Magharibi mwa Tanzania.
Mkurugenzi wa
mawasiliano jimboni humo Mchungaji Dkt Joseph Otieno amesema kuwa viongozi
wa ngazi ya unioni ya kaskazini mwa Tanzania akiwamo Mchungaji Daktari
Godwin Lekundayo, na Katibu wake
Mchungaji Daudi Makoye wamewasili jimboni humo kwa ajili ya usimamizi wa mkutano huo.
Eneo la Konferensi hiyo linalojumuisha Mkoa wa Mara na Kisiwa cha Ukerewe kilichoko katika Ziwa Victoria lilianzishwa na kanisa la Waadventista Wa Sabato mwaka 1909,kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014 eneo hilo lina makanisa 387 yenye waumini wapatao 124,954 katika eneo hilo lenye wakazi 2,795,493
Post a Comment