MTANGAZAJI

ARUSHA:MKUTANO MKUU WA KONFERENSI YA KASKAZINI MASHARIKI MWA TANZANIA (NETC) KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WAANZA


Mch Zawadi Kajiru - Katibu Mkuu akitoa ukaribisho na matangazo mbalimbali.

Kwaya ya Ngongongare ikiimba

Kwaya ya Magadirisho nayo ilikuwepo


Mkutano Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika Konferensi ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania (NETC) umeanza jana jioni katika Chuo Kikuu cha Arusha (UOA) ukihudhuriwa na wajumbe takribani 600 toka Arusha,Kilimanjaro,Tanga na Manyara.

Mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano unalengo la kuweka mikakati mbalimbali ya kazi na kuchagua viongozi watakaoongoza konferensi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na unatarajiwa kumalizika Septemba 15 mwaka huu.

NETC ni miongoni mwa konferensi nne zinazounda Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania ambayo ilifanya mkutano wake mkuu uliomalizika hivi karibuni.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.