MTANGAZAJI

ZIARA YA WAIMBAJI WA LIGHTBEARERS JIJINI NAIROBI NA MWANZA


Kundi zima la waimbaji wa Light Bearers toka jijini Dar es salaam katika studio za JCB watakuwa na ziara ya nchini Kenya katika jiji la Nairobi mwishoni mwa juma hili Agosti 29 na 30,2015 ambapo watashiriki kwenye tamasha lililoandaliwa na mwimbaji Israel Mugisha wa jijini humo.

Baada ya Tamasha hilo wataelekea jijini Mwanza kwenye Tamasha lingine ambalo litafanyika katika ukumbi wa Vijana Septemba 5,2015 ziara hiyo itaambatana na uzinduzi wa toleo lao jipya namba 3.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.