IRINGA:WANANCHI WAILALAMIKIA SERIKALI KUHUSU KERO YA MAJI
Wananchi wa vijiji vya Ilole,kitumbuka,Ilambilole,Ikengeza,Chamdindi na vingine vilivyopo Katika wilaya ya
Kilolo na Ismani mkoani Iringa wameilalamikia serikali kwa
kushindwa kutatua kero ya maji iliyodumu kwa muda mrefu katika maeneo hayo.
Wakizungumza kwa huzuni mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
aliyefanya ziara ya kukagua miradi ya maji Katika wilaya hizo Amina Masenza
wananchi hao wamesema kumekuwa na ubabaishaji wa kisiasa juu ya namna ya
kupelekewa maji jambo ambalo linawafanya waweze kutumia maji yasiyo salama kwa
afya zao.
Akijibu kero za wananchi hao Mkuu wa mkoa Amina Masenza
amesema kumekuwa na watumishi wa serikali ambao wamepelekwa kusomea utalamu huo
lakini bado hawafanyi kazi sawasawa na elimu zao ambapo ameahidi
kulishughulikia jimbo hilo pamoja na kusimamia miradi mipya iliyopo ili iweze
kuwanufaisha wananchi kwa kupata huduma hiyo kwa urahisi.
Kwa upande wake mhandisi wa Maji na meneja mradi wa Maji
vijijini Andrew Kisaru amesema kwasasa wanaongeza nguvu ya udhibiti wa
matumizi ya maji kwa kufunga mita kwani kwa sasa Katika jimbo la ismani idadi
ya watumiaji inakaribia 15000 ambapo kila kaya inaweza kulipa kiasi cha sh 5000
kwa mwaka ambapo tayari Unit 267 zimefungwa katika maeneo hayo hivyo
amewahakikishia wananchi kwa tatizo na kero hiyo ya maji itamalizika kwa wakati
muafaka
Post a Comment