DAR ES SALAAM:TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TANZANIA YAPONGEZWA
Dr.Benson Banna |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imeelezwa kuwa imeweka historia na kujenga
heshima ya taifa kwa kuweza kuandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kwa Mfumo wa BVR kwa mafanikio na kuyashangaza mataifa
makubwa duniani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kufuatilia Masuala ya Uchaguzi
Tanzania (TEMCO), ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Kufuatilia Masuala ya
Uchaguzi, Dr Benson Banna, amesema kuwa NEC inastahili pongezi kubwa kwa hatua
hiyo.
Amesema utafiti uliofanywa na Temco kwa kupitia vituo 8,398
vya uandikishaji ambavyo ni asilimia 80.5 ya vituo vyote, umedhihirisha kuwa
kazi hiyo ilifanyika kwa ukamilifu kwa wananchi wengi kupata nafasi ya
kujiandikisha huku asilimia 64 ya vituo vikizidisha hadi muda wa kufunga katika
kuwawezesha wananchi kujiandikisha.
Kwa hatua hiyo, Dk Banna amesema NEC imefuta aibu kwa Taifa,
kutokana na mataifa mbalimbali ya nje kubeza uwezo wa nchi katika kufanikisha
uandikishaji huo kabla ya kuanza na kwamba sasa kama Taifa, Tanzania imeanza
kuonesha uwezo mkubwa wa kujitegemea katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi.
Amesema wakati tathimini ya awali ilikuwa ni kuhitajika kwa
visanduku vya BVR zaidi ya 15, 000, serikali ilikataa pendekezo hilo na kusema
visanduku vinavyohitajika ni 14,000, lakini hata hivyo havikuweza kununuliwa
badala yake vilinunuliwa visanduku 8,000 tofauti na ushauri wa NEC ambayo
ilishauli kiwango cha chini kiwe visanduku 10,000
Post a Comment