DAR ES SALAAM:VYOMBO VYA HABARI NCHINI TANZANIA VYATAKIWA KUSIMAMIA WAJIBU WAKE WAKATI WA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU
Waandishi wa habari wakitekeleza majukumu yao |
Vyombo vya habari nchini Tanzania vimetakiwa kuhakikisha vinasimamia wajibu wake ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na wa haki.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora (CEGODETA), Thomas Mgawaiya wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuandika na kufuatilia habari za Uchaguzi Mkuu.
Programu ya mafunzo hayo imeandaliwa na Shirika la Habari la Kimataifa la Internews ambapo itadumu kwa muda wa miezi 18.
Amesema vyombo vya habari havitakiwi kupendelea au kuvibagua baadhi ya vyama vya siasa na wagombea, kutopokea rushwa, kutoandika habari za uchochezi, chuki na uhasama baina ya vyama vya siasa na wagombea na kutofanya hivyo baada ya matokeo rasmi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania(NEC).
Post a Comment