DAR ES SALAAM:MABASI YAENDAYO HARAKA YAANZA SAFARI
Mabasi
maalumu kwa ajili ya kutoa huduma chini ya mradi wa mabasi yaendayo haraka
yameingia nchini tayari kwa kuanza huduma ambapo leo Agosti 17 yamefanya safari Kutoka Ubungo kwenda Kimara na kutoka Kimara hadi kivukoni Bure.
Mbali na kuanza kwa huduma ya mabasi hayo Kampuni
ya ubia ya UDART kwa kushirikiana na wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) pia
inaanza leo kuendesha mafunzo kwa madereva kabla ya huduma ya usafiri kuanza
rasmi Oktoba.
Meneja wa Udart, Sabri Mabruk amesema Ujio wa mabasi hayo na kuanza
kwa huduma zake, ndiyo mwisho wa daladala za kawaida kati ya Kimara na
Kivukoni na kuongeza kuwa kutakuwa na
utaratibu wa kulipa gharama za usumbufu kwa wenye mabasi ya daladala na kisha kuwapangia
njia nyingine.
Mabruk
amesema Baada ya mafunzo ya wiki mbili kwa madereva, mabasi yaliyoko yatatoa
huduma kupitia vituo 10 pekee kabla ya Septemba ambayo idadi ya mabasi itakuwa
imekamilika.
Mabasi
hayo yanayotarajiwa kutumia dakika 20 kutoka Kimara hadi Kivukoni eneo la
Magogoni ambapo ndani yana viti kwa ajili ya wazee, wajawazito wenye, ulemavu
na mikanda maalumu ya kushika kwa abiria wanaosimama.
Post a Comment