DAR ES SALAAM:UHAKIKI WA TAARIFA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA SASA AGOSTI 18 HADI 22 MWAKA HUU
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesogeza mbele uhakiki wa taarifa za uandikishaji
wananchi katika daftari la wapigakura kwa kutumia mfumo wa BVR kwa Mkoa wa Dar
es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Ramadhani Kailima amesema kuanza
uhakiki taarifa za wakazi wa mkoa huo waliojiandikisha katika daftari hilo,
utaanza Agosti 18 hadi 22, mwaka huu.
Wiki
iliyopita NEC ilitangaza kuanza kuhakiki kwa taarifa za wapiga kura kwa mkoa
huo Agosti 15 hadi 19, mwaka huu.
Kailima
amesema hatua hiyo inatokana na changamoto za mifumo ya uchakataji wa taarifa
za wapigakura ili kuondoa mapungufu yanayoweza kujitokeza na kuchukua muda
wa kukamilisha uchapaji wa daftari la
awali la wapigakura kwa mkoa huo.
Amesema
kutokana na changamoto hizo, Tume inawatangazia wakazi wa mkoa huo kuwa daftari
hilo litawekwa wazi kwa ajili ya kukaguliwa kuanzia kesho hadi Jumamosi ijayo.
Post a Comment