ARUSHA:WAFANYABIASHARA WALALAMIKIA TATIZO LA KUKATIKA KWA UMEME
Wafanyabiashara
mkoa wa Arusha hasa wanaouza barafu, samaki, na nyama wamelalamikia kitendo cha
kukatika umeme mara kwa mara kwa muda wa zaidi ya mwezi sasa hali inayosababisha
bidhaa zao kuharibika.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakazi wa jiji la arusha wamesema kuwa tangu mwishoni mwa
mwezi wa 7 tatizo hilo lilianza kujitokeza hadi sasa bila kupatiwa ufumbuzi.
Aidha
kutokana na hali hiyo Afisa Uhusiano wa Tanesco mkoa wa Arusha, Fredy Robert,
amekiri kuwepo kwa tatizo hilo huku akisema kuwa taizo hilo linatokana na
marekebisho yanayofanyika katika maeneo mabalimbali nchini.
Blog hii imeshuhudia keleleza za jenereta katika maeneo mbalimbali jijini
humo hasa maeneo ya biashara.
Post a Comment