ARUSHA:WAIMBAJI WA THE LIVING VOICES TOKA KAMPALA,UGANDA WAKO JIJINI ARUSHA
The Living Voices wakiimba hii leo katika ufunguzi wa makambi ya Sakina,Arusha |
Msimu wa mikutano ya makambi ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani
kote hufanyika kuanzia mwezi julai hadi Septemba kwa muda wa siku
saba kwa kuwakutanisha waumini wa kanisa hilo katika makanisa yao ikiwa na lengo la kuwaimarisha kiroho.Ni
utaratibu wa kanisa hilo toka enzi na enzi kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia wanayoyaamini.
Mikutano hiyo ya makambi huwapatia fursa waimbaji wa vikundi,mmoja mmoja ama kwaya kualikwa kutoka eneo moja kwenda jingine iwe ni kanisa mahalia,wilaya,mkoa ama nje ya nchi.
Makambi ya Sakina jijini Arusha mwaka huu wa 2015 yanahudumiwa na waimbaji wa The Living Voices toka Kampala Uganda wakishirikiana na kwaya zingine za hapo ikiwemo kwaya ya Vijana na kwaya ya kanisa la Sakina.
The Living Voices ni kwaya inayoundwa na waimbaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato jijini Kampala ambao wanatoka katika makanisa mbalimbali ya Waadventista Wa Sabato jijini humo na miongoni mwao ni mke wa Mwalimu wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Rwanda Mwalimu Sozzy Joram ambaye anaimba sauti ya pili katika kwaya hiyo.
Post a Comment