MAKAMBI YA MZIZIMA YAFANYIKA NJE YA JIJI LA DAR ES SALAAM NA KUFANA
Msimu wa Makambi ya kila mwaka ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato unaendelea katika sehemu mbalimbali duniani.
Pichani ni katika Makambi ya Kanisa la Mzizima jijini Dar es salaam ambapo yalifanyika Juni 28-Julai 4, 2015 huko Magodani,Vikindu ambako ni nje ya jiji Dar es salaam kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hapa nchini ambapo waumini wa kanisa hilo duniani hufanya makambi nje ya maeneo yao wanayoishi na makanisa mahalia japo utaratibu huo bado unatumiwa na waumini wake walioko katika nchini, nchi kadhaa hasa barani Ulaya na Marekani.
Huku makanisa mengine hasa yaliyoko mijini nchini Tanzania yakikabiliwa na changamoto ya kufanya makambi kwenye makanisa yao.
Wachungaji waliohudumu ni Rahisi Mande,Peter Mumbara, Mages Mabu na Baraka Butoke(Mchungaji wa Mzizima )
Kwaya ngeni ilikuwa ni ya Ifakara Morogoro na kwaya wenyeji walikuwa ni TUCASA MUHAS, Wazee na TUCASA IFM.
Kwaya ya Mzizima ikiimba |
Kwaya ya Ifakara Morogoro |
Mch Baraka Butoke akiimbisha kwaya ya Wazee |
Kwaya ya TUCASA MUHAS |
Watoto |
Post a Comment