HIZI NDIZO FURSA ZILIZOPO TANZANIA ALIZOZITAJA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA
Juni 18 mwaka huu Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing wakati wa Kongamano la kampuni ya mawasilino ya HUAWEI toka China lililofanyika jijini Dar es salaam amesema Tanzania ina fursa mbalimbali ambazo zikitumika zaweza kuleta maendeleo katika nchi hiyo.
Kwanza ni masuala ya utalii kutokana na wingi wa mbuga za wanyama na hifadhi za zaifa zilizoko nchini na utamaduni wa wananchi wa Tanzania wanaotoka katika makabila zaidi ya 120.
Pili suala la kuwa na viwanda ambavyo kwa sasa vimepungua hivyo linahitaji kushirikisha wadau wa ndani na nje ya nchi katika kuwekeza kwenye viwanda.
Akaeleza kuwa hali ya amani nchini tofauti na nchi zingine ni miongoni mwa fursa ambayo inaweza kutumiwa na viongozi na wananchi wa Tanzania katika kujiletea maendeleo japo alisisitiza kuwa masuala hayo ili yaweze kufanikiwa kwa sasa serikali ya Tanzania na wadau mbalimbali wanapaswa kushirikiana katika kuwekeza kwenye miundo mbinu ya teknolojia ya habari na mawasilino (Teknohama) kama ilivyo huko Uchina.
Post a Comment