MTANGAZAJI

MTUHUMIWA WA MAUAJI KANISANI MAREKANI ALIPEWA ZAWADI YA BUNDUKI NA BABA YAKE

 

Shirika la Utangazaji na BBC kupitia kipindi chake cha Focus On Africa usiku wa leo kwa lugha limeeleza kuwa mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la kihistoria mjini Carolina Kusini amekamatwa na alitumia bunduki aliyopewa zawadi na baba yake katika maadhimisho ya siku yake ya  kuzaliwa.

Kulingana na mwanasheria mkuu Lorreta Lynch,awali maafisa walimtaja kijana huyo wa miaka 21 kuwa Dylann Storm kama mtu waliyekuwa wakimsaka kwa shambulizi la Charleston.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami na bunduki aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo.

Maafisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki.
Bi Lynch amesema idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini njia mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.
 
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa bwana Storm alikamatwa huko Selby Carolina kaskazini saa 13 baada ya shambulizi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.