DAR ES SALAAM:MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA NCHINI TANZANIA MWAKA 2014 YAMETANGAZWA
Baraza La Mitihani Tanzania limetoa
taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Septemba 10 hadi 11 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dr Charles E. Msonde amesema jumla ya watahiniwa 808,085 wa shule za msingi waliosajiliwa kufanya mtihani huo waliofanya ni watahiniwa 792,122 waliofaulu ni watahiniwa 451,392 sawa na asilimia 56.99 kati ya hao wasichana
ni 226,483 na wavulana ni 224,909.
Dr Msonde amesema takwimu za matokeo zinaonesha kuwa
ufaulu katika matokeo yote umepanda
ikilinganishwa na mwaka 2013. watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la
kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 69.70 na somo walilofaulu kwa kiwango cha
chini ni hisabati lenye ufaulu wa aslimia 37.56.
Baraza la mitihani la Tanzania
limefuta matokeo yote ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2014 ya mtahiniwa mmoja aliyebainika kufanya udanganyifu katika mtihani
huo na kusema kuwa idadi ni ndogo ikilinganishwa na watahiniwa 13 walifutiwa
matokeo mwaka 2013.
Msonde amesema matokeo hayo yamewekwa
kwenye tovuti za baraza la mitihani,
wizara ya elimu na mafunzo na ofisi ya waziri mkuu tamisemi ili kila mtahiniwa
aweze kuona matokeo yake.
Post a Comment