DAR ES SALAAM: ANGEL MAGOTI AMPA RAIS KIKWETE CD YAKE YA NYIMBO ZA INJILI
Angel Magoti akiwa na Rais wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete na hapa wakiwa wameshika audio-cd ya mwimbaji huyo |
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka Kanisa la Waadventista Wa Sabato Temeke Angel Magoti Jumatatu ya juma hili alipata nafasi ya kuimba wimbo ulio na maudhui ya ya kupambana na kuzuia rushwa.
Angel ambaye pia ni mwimbaji wa Kwaya ya Vijana ya kanisa hilo aliimba wakati Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete alipofungua mkutano wa 12 wa shirikisho la Taasisi za kupambana
na kuzuia Rushwa kwa nchi za SADC katika Hoteli ya Malaika iliyopo
jijini Mwanza.
Baada ya hapo Angel mwenye matoleo mawili ya nyimbo za injili toka aanze kuimba peke yake na ambaye wazazi wake wote ni waimbaji huku mama yake akiwa ni miongoni mwa waimbaji wa kwaya ya kanisa la Temeke alimkabidhi Rais Jakaya Kikwete audio cd yake ya toleo namba mbili yenye nyimbo 10 alilolitoa mwaka huu wa 2014 liitwalo Umefanya Tena.
Katika tukio hilo Angel Magoti ambaye pia ni mwimbaji wa TM Music alikuwa ameambatana na Mwalimu wa nyimbo za Injili Tumaini Lameck Murungu.
Picha zote na Injilileo Blog |
Post a Comment