MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:VIONGOZI WA MORNING STAR TELEVISHENI KUKUTANA NA WADAU KESHO


Uongozi wa Morning Star Televisheni kesho utakutana na wadau mbalimbali wa kituo hicho wa jijini Dar es salaam ili kufanikisha maendeleo yake.

Mkutano huo utakaofanyika katika makanisa ya Waadventista Wa Sabato Mwenge,Ilala na Ukonga kuanzia saa 9 alasiri.

 Mkurugenzi wa kituo cha Morning Star Televisheni Mr.Mazara Edward Matucha  amesema hivi karibuni kuwa  tukio hilo litakuwa na lengo la kutoa shukrani kwa wadau wa kituo hicho ambacho sasa kiko katika majaribio ambapo kutakuwa na kubadilishana kwa mawazo baina ya wadau wa Mstv na viongozi wa Mstv kwa maongezi ya ana kwa ana kwa mrejesho wa kile kilichofanyika na ambacho kimefanyika na mipango ya sasa juu ya runinga hii.

Amesema siku hiyo itakuwa nzuri na maalum kwa kutoa mwanya kwa watu binafsi au familia kuwa marafiki wa Mstv kwa kuchukua kadi maalum za kuchangia kazi za Mstv kwa mpango,ambako mchangiaji anaweza kuamua kuchangia kwa muda anaotaka na kuelekezwa  ya namna ya kuwasilisha mchango huo.


Matucha amefafanua kuwa watajenga mtandao  wa marafiki Mstv ili kuleta  ukaribu kwao kujua nini kinafanyika lini na wapi,na kupata mialiko kadhaa toka Mstv inapotokea hitaji la kufanya  hivyo.

Mkurugenzi wa kituo cha Morning Star Televisheni Mazara Edward Matucha (Picha na Injili blog)No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.