UKEREWE:WAADVENTISTA WA SABATO WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MJI WA NANSIO HII LEO
Washiriki wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato wanaoendesha mkutano wa injili katika mji wa Nansio wilayani
Ukerewe leo wamefanya usafi wa mazingira katika mji huo na viunga vyake.
Akizungumza na morning star
radio hii leo mkurugenzi wa idara ya vijana ya kanisa la waadventista wasabato
union comferensi ya kaskazini mwa Tanzania mchungaji Elius Kasika anaye endesha mkutano huo kwa
kushirikiana na kwaya nane amesema kuwa
tukio hilo la kusafisha mji ni moja ya shughuli zilizopangwa na mkutano huo kwa
kuwa leo ni siku ya usafi katika mji huo.
Waimbaji walioko kwenye
mkutano huo wanatoka katika kwaya za Miembeni,Bunda mjini,Misongwi,Shinyanga,Kahama
Mjini,Baso,Nyashimba na TUCASA-Sauti.
Kasika amesema lengo la
utaratibu huo wakufanya usafi wa mazingira nikuonyesha kanisa kuwa ni sehemu ya
jamii hivyo inalo wajibu wakushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii
ikwemo maswala ya usafi.
Mkutano huo ulioanza julai 3
ukiwa unadhaminiwa na chama cha wanafunzi wanaosoma kwenye vyuo vya kati na
vyuo vikuu wa kanisa la waadventista wasabato nchini (TUCASA) kwa kushirikiana
na washiriki wa makanisa ya Nansio,mjini kati,Bukonye,Mulezi,Amkoko,Pilimagule,Butoni
na Namagubo kwa lengo lakutoa mafundisho ya afya, familia na kiroho.
Post a Comment