TARIME:WAKAZI WA INANO WAITAKA SERIKALI KUONGEZA WALIMU WA SAYANSI
Wakazi wa Tarafa ya Inano wilayani Tarime wameitaka
serikali kuongeza walimu wa masomo ya sayansi katika shule ya sekondari ya Manga ili kuweza kuwanusuru
wanafunzi walioko katika shule hiyo wasiendelee kupoteza muda wao wa kuhudhuria
masoma bila ya walimu wa masomo hayo .
Mkuu wa shule hiyo Victoria
Yonas amesema kuwa shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu ya wananchi ina upungufu
mkubwa wa idadi ya walimu hasa wamasomo ya sayansi licha ya kubahatika kuwa na
vitabu vya kutosha kwaajili ya kufundishia na kujifunzia pamoja na vya rejea.
Shule hiyo inayotakiwa
kupewa hadhi ya kuwa nakidato cha tano na sita imekumbwa na tatizo la kutokamilika
kwa mabweni na ukosefu wa vyoo .
Kilio hicho kimetolewa wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Tarime Nyambari
Nyangwine alipokuwa akifanya mkutano katika viwanja vya shule ya sekondari hiyo
iliyopo katika kata ya Manga Wilayani Tarime.
Nyangwine amesema kuwa
tatizo la upungufu wa walimu wasayansi ni la nchi nzima na serikali inajaribu
kuweka kipaumbele kwa walimu wa masomo ya sayansi ili kuwavutia wanaopenda
kusoma masomo hayo wapate nafasi za upendeleo kuongeza idadi iliyopo ili
kupunguza tatizo hilo.
Post a Comment