MTANGAZAJI

MARA:WATATU WAHUKUMIWA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUMILIKI NYARA ZA SERIKALI


Mahakama ya Wilaya ya Tarime imewahukumu watu watatu, wakiwemo raia wawili wa nchi jirani ya Kenya  miaka 20 jela kila mmoja baada ya kuwakuta na kosa la kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria wilayani Tarime Mkoani Mara.

Waliohukumiwa ni Fred Opiso Mweri (29) Mkisii na mfamasia katika kituo cha afya cha Masanga, Ruben Kerero Moseri (40) mkisii na mkazi wa Isibania nchini Kenya na Nyambari Mahunda Sabai (26) mkazi wa Masanga huku ikimwachia huru mwalimu Thomas Ryoba Nyariese(62) wa shule ya msingi ya Catherine iliyoko Masanga wilayani humo.

Wote kwa pamoja walikutwa na kosa moja  la kuhujumu uchumi kwa kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, ngozi ya chui na kipande cha jino la Tembo, zenye thamani ya  shilingi  6 milioni kwa pamoja .

Hukumu hiyo ilitolewa julai 21 na iliyochukuwa takribani saa 1:30 kusomwa na hakimu Odira Amworo , washitakiwa walipewa nafasi ya kujitetea  kwa wakati tofauti ambao walisema wanaumwa na ni mara yao ya kwanza hivyo wakaiomboa mahakama kuwapunguzia adhabu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.