MTANGAZAJI

UHOLANZI:MMOJA WA VIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ALIBADILISHA TIKETI DAKIKA CHACHE KABLA NDEGE ILIYODUNGULIWA KUONDOKA



Kanisa la Waadventista la Waadventista Wa Sabato nchini Uholanzi limesema mmoja wa viongozi wa kanisa hilo alinusurika kuhusika kwenye ajali ya ndege ya Malaysia baada ya kubadilisha tiketi ya  kusafiri na ndege hiyo iliyodunguliwa huko Mashariki mwa Ukraine juma lililopita na kuua watu 298 papo hapo.

Mwenyekiti wa Unioni Konferensi ya Uholanzi Wim Altink amesema jana kuwa Frieda Souhuwat-Tomasoa alikuwa amekata tiketi ya ndege hiyo namba 17 kutoka Amsterdam  kuelekea mji mkuu wa Malaysia Julai 17 mwaka huu lakini alibadilisha tiketi dakika chache kabla ya kuondoka kwa ndege hiyo na kuamua kusafiri na ndege ya shirika la ndege la Emirates. 

Souhuwat-Tomasoa ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Unioni konferensi ya Uholanzi na mzee wa kanisa la Rotterdam Kaskazini alikuwa akisafiri kuelekea Ambon,Indonesia kwa ajili ya kuusaidia umoja wa mataifa kwa ajili ya kushughurikia mgogoro wa kidini uliodumu katika eneo hilo kwa muda wa miaka 10 sasa.  

Souhuwat-Tomasoa  kwa sasa yuko Moluccas, Indonesia na amekuwa akisafiri kuelekea Ambon katika visiwa vya Maluku vilivyoko mashariki mwa kisiwa cha Sulawesi akiwa ni mjumbe wa umoja wa mataifa kwenye mpango huo. 

Taarifa zinaeleza kuwa mbili ya tatu ya abiria waliopanda ndege hiyo ni raia wa uholanzi ambako julai 21,mwaka huu viongozi wa makanisa walishiriki kwenye maombi ya maalum ya kuwaombea waliopoteza ndugu na jamaa kwenye ajali hiyo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.