MARA:MWANAMKE AUAWA KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI
Mwanamke
aliyetambulika kwa jina la Mariam Matiko (20) mkazi wa Kitongoji cha Romboni
kijiji cha Nyangoto katika mji wa Nyamongo wilayani Tarime amekutwa amefariki
dunia ndani ya nyumba yake akiwa ametapakaa damu mwili mzima bila kuwa na
jeraha lolote.
Tukio hilo lilitokea julai 18 mnamo saa 7.30 wakati
majirani walipogundua kuwa dada huyo alikuwa haonekani kwa masaa kadhaa kisha
kutoa taarifa kituo cha polisi cha Nyangoto ambao walifika eneo hilo kwa
ukaguzi na kumkuta mwanamke huyo akiwa amefariki huku amefungwa khanga
shingoni.Mumewe mariamu alitajwa kuwa ni Mwita Mtumba anayedaiwa kuwa alimuua
mkewe kutokana na wivu wa mapenzi kwa kumhisi kuwa na mahusiano na mwanamume
mwingine na hili ni tukio la pili katika eneo la Nyamongo baada ya lile la
mwanamke kuchomwa sehemu zake siri na mwanaume.
Kwa mjibu wa
taarifa ya Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Nyamongo Kagumilwa Kaijage kwa
ushirikiano na jeshi la polisi, ukaguzi uliofanywa unaonesha marehemu alikuwa
mekaa kwenye kiti akiwa amefungwa khanga shingoni, lakini haikuonekana kuwa ana
alama yoyote ya kujinyonga na ndipo
mwili ulipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kilichoko kituo cha afya
Nyamongo lakini ndugu wa marehemu walimchukuwa na kwenda kumzika baada ya
kuelewana na upande wa mwanamume watalipa ng’ombe watano.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Tarime
Rorya kamishina msaidizi Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa mtuhumiwa baada ya kutenda kosa hilo alitorokea kusiko julikana
na jeshi la polishi linafanya juhudi za kumtia mbaroni.
Post a Comment