MTANGAZAJI

IRINGA:WANAWAKE WATAKIWA KUPIMA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZIWanawake   Mkoani  Iringa nchini Tanzania  wametakiwa kuchukua tahadhari  kwa  kupima  magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani  ya mlango  wa kizazi, ugonjwa  unaoonekana kuwa tishio kwa wanawake wengi nchini humo.

Akizungumza  na wandishi wa habari ofisini kwake , Mwenyekiti  wa mabalozi wa wahudumu wa kujitolea  katika  shirika la  (TALWORK) Mkoani Iringa  Bw Nasri  Mwampeta  amesema kuwa takwimu zinaonyesha  kuwa wanawake wawili  hufariki kila mwezi Mkoani humo kutokana na ugonjwa huo ambapo kwa mwaka hufariki wanawake 24.

Amesema kuwa  ugonjwa  huo unatokana na  virusi  aina ya  Human  Papiloma Virus (H.P.V) ambavyo huambukizwa  kwa njia ya kujamiiana.

Aidha  amesema kuwa   ugonjwa huo  unawapata wanawake  walio na umri  wa miaka (25-50) ambapo hauna dalili  kwani hukaa  miaka  (10-20)  baada ya hapo ndipo dalili zinaanza kujitokeza.

Hata hivyo wanawake wanatakiwa  kujitokeza kwa  wingi  kupima   ugonjwa huo unatibika  bila  gharama yoyote  katika vituo mbalimbali Mkoani Iringa  ikiwemo Hospitali ya Mkoa,   kituo  cha  afya Ipogoro,  Marie   Stopers  na hospitali ya Ipamba.moja ya  visababishi  vya  ugonjwa huo  ni utumiaji wa  bidhaa za tumbaku, kuzaa watoto zaidi  ya watano, kujamiiana katika umri mdogo .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.