MTANGAZAJI

BRAZIL:KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO NCHINI BRAZIL KUTOA HUDUMA ZA KIROHO NA KIJAMII WAKATI WA KOMBE LA DUNIA



 

 Makanisa mahalia ya Waadventista Wa Sabato nchini  Brazil yatashiriki  kutoa huduma za kiroho na kijamii kwa maelfu ya mashabiki wa mchezo wa soka wakati wa mashindano ya kombe la dunia  yanayotarajiwa kuanza nchini humo juni 12,mwaka huu.

Shirika la Habari la Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani (ANN) limeeleza kuwa ,Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Brazil limepanga kuwatumia vijana na watu wazima wa kanisa hilo katika majiji 12 inakofanyika michuano hiyo kwa kutoa huduma ya maji,matamasha ya uimbaji,maonesho ya masuala ya afya na kujitolea damu.

Mpango huo unaoitwa Tumaini kwa Brazil unalengo la kuwafikia watu toka nchi mbalimbali duniani watakaokuwa  Brazil kushuhudia mashindano hayo  pia utahusisha usambazaji wa vipeperushi na uuzaji wa beji nchini humo ambako shule zitakuwa zimefungwa kwa muda wa siku 32 za michuano hiyo.

Hata hivyo kutakuwa na ugawaji wa vitabu  milioni moja   vya Tumaini Pekee kilichoandikwa na mwinjilisti wa  Alejandro Bullón,magazeti yanayozungumzia matatizo ya biashara ya ngono. 

Areli Barbosa, ambaye ni Mkurugenzi wa Vijana wa Divisheni ya Amerika ya Kusini katika kanisa la Waadventista Wa Sabato amesema mpango huo si kwa ajili ya kuunga mkono michuano ya soka ya Kombe la Dunia bali ni kutoa huduma kwa jamii.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.