DAR ES SALAAM:JWTZ KUFANYA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) limeeleza kuwa linatarajia kufanya kongamano
kubwa la Kijeshi linalokwenda sanjari na
maonyesho ya Zana za kijeshi Jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam,Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu,Meja
Jeneral Mustafa Kejuu,Ameeleza kuwa kongamano hilo litafanyika Julai 14 hadi 16
katika ukumbi wa Mkutano wa Mlimani
City.
Ameeleza maonyesho hayo Yatatoa Fursa kwa Washiriki
toka Kada Mbalimbali kubadilishana mawazo,kuona na Kutangaza Biashara ya zana
za kijeshi.
Aidha Ameeleza kuwa Majeshi Yatakutana Kujadili
Namna ya Kukabiliana na changamoto za sasa Za ulinzi Na Usalama wa Dunia
Hususani Eneo la Afrika Mashariki ambalo linakabiliwa na changamoto mbalimbali
Ikiwemo Uvuvi haramu Uharamia na Jinsi Ya kulinda Maliasili Za Taifa.
Kongamano Hilo litaleta Wajumbe kutoka SADC,Umoja wa
Afrika na jumuiya Nyingine za Kimataifa kujadili na kutatua changamoto
mbalimbali za ulinzi na usalama na kuweka Mikakati Ya Pamoja kuimarisha Ulinzi
na usalama Duniani.
Post a Comment