MARA:KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WIKI NZIMA WILAYANI SERENGETI
Kituo cha sheria na
haki za binadamu kupitia mawakili na wana sheria wake kwa kushirikiana na
wasaidizi wa kisheria na haki za binadamu wilayani Serengeti mkoani Mara
wameanza wiki ya msaada wa kisheria bure kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Mwanasheria kutoka
kituo hicho Rodrick Kimaro amesema lengo nikutoa msaada wa kisheria bure kwa
jamii kuhusiana na maswala ya kisheria,
ushauri,na kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria na haki za binadamu
kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wakupata haki.
Aidha wananchi
wenye matatizo mbalimbali ya kisheria wilayani Serengeti,wajitokeze julai 5
mwaka huu ili waweze kupewa msaada wa kisheria na ushauri.
Mwenye kiti wa
shirika la wasaidizi wa kisheria na haki za binadamu wilayani Serengeti Samuel
Mewama amesema huduma hiyo ambayo imekuwa ikitolewa kila mwaka imesaidia
wananchi kujua haki zao na kuzidai na hivyo kuimarisha utawala bora. Katika
zoezi kama hilo mwaka jana migogoro
mingi ulihusu miradhi,ukatili wa
kijinsia,migogoro ya ardhi na ndoa.
Post a Comment