VIJANA 25 WA KITANZANIA WAHUKUMIWA ADHABU YA KIFO CHINA
Takribani
vijana 65 wa Kitanzania wamehukumiwa adhabu ya kifo huko nchini China baada ya
kupatikana na hatia ya kujihusisha na
dawa za kulevya.
Vijana hao
ni kati ya zaidi ya 403 wa Tanzania wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali
duniani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hizo.
Hayo
yamesemwa hapo jana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(sera utaratibu na
Bunge)William Lukuvi,mjini Dodoma wakati akizungumzia maadhimisho ya siku ya
Dawa za kulevya Duniani yanayofanyika juni 26 kila mwaka.
Lukuvi
amesema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho ya kesho,kitaifa yatafanyika katika viwanja
vya shule ya msingi Nzovwe jijini Mbeya na Makamu wa Rais,Dk Gharib
Bilal,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Amezitaja baadhi
nchi ambako vijana wanashikiliwa kuwa ni Brazil(108),Hong kong (118),Kenya(34),Pakistan(16)na
China 65.
Post a Comment