MTANGAZAJI

IDADI YA WANAOUGUA HOMA YA DENGUE NCHINI TANZANIA YAONGEZEKAIdadi ya Watu waliougua ugonjwa wa homa ya  dengue nchini Tanzania kuanzia Januari mwaka huu hadi juzi imefikia watu 376 .

Mtaalamu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dr Janeth Mugamba amewaambia waandishi wa habari kuwa  hadi jana watu wawili walikuwa wamepoteza maisha,idadi ambayo amesema kuwa inaweza kuongezeka endapo upimaji utafanyika kwenye kila wilaya na kuahidi kutoa taarifa zaidi kesho.

Amesema Wilaya ya Kinondoni ina wagonjwa wengi zaidi, ikifuatiwa na Ilala na Temeke. Hata hivyo, amesema huenda wilaya zenye idadi ndogo ya wagonjwa hazijaweza kupima na kubaini watu wenye maradhi hayo ikilinganishwa na Kinondoni.

Juzi, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema hali ni mbaya na wananchi wanatakiwa kuchukua hadhari wasipate maambukizi ya ugonjwa huo.

Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa  maambukizi ya homa ya dengue hutokea baada ya mtu mwenye ugonjwa huo kuumwa na mbu  aina ya Aedes Egyptiae na mbu hao wakichukua virusi, huvisambaza kwa watu wengine.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.