MTANGAZAJI

DENI LA TANZANIA LAFIKIA TRILIONI 21.2Deni  la Taifa la Tanzania limeendelea kuongezeka na sasa limefikia Sh. trilioni 21.2 kiwango ambacho kama kikigawanywa kwa kila Mtanzania wanaofikia milioni 45  kwa usawa, kila mmoja atatakiwa kulipa Sh. 471,111.

Kiwango hicho cha deni kimepanda kutoka Sh. trilioni 16.98 cha mwaka wa fedha 2011/12.

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alitoa taarifa ya deni hilo jana kwa waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu ripoti ya ukaguzi iliyowasilishwa bungeni ya mwaka wa fedha wa fedha 2012/13 ambayo inaishia Juni 30, mwaka jana.

Utouh alisema ongezeko hilo limesababishwa na mikopo kutoka kwenye mabenki na nchi wafadhili kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo nchini Tanzania.

Utouh amefanunua kuwa  deni la nje limefikia Sh. trilioni 15 hadi Juni 30, 2013  ambalo ni ongezeko la Sh. trilioni 3.0 kutoka Sh. trilioni 12.43 kwa mwaka 2011/12, wakati lile la ndani limefikia Sh. trilioni 5.78 ikiwa ni ongezeko la Sh. trilioni 1.23 kutoka Sh. trilioni 4.55 kwa mwaka 2011/12.
Akizungumzia misamaha ya kodi, CAG amesema ukaguzi huo umebaini kuwa hadi kufikia Juni 30, mwaka jana Sh. trilioni 1.52 zilitolewa kama misamaha ya kodi.
 Amesema mwenendo umeonyesha kuwa kiasi hicho kimepungua kutoka Sh. trilioni 1.81 mwaka 2011/12 hadi Sh. trilioni 1.52 mwaka 2012/13 ambao ni upungufu wa Sh. bilioni 290.60 (asilimia 16).


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.