WAKUU WA MIKOA YA SHINYANGA NA TABORA WAUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MGOGORO WA ARDHI
Wakuu wa Mikoa ya Shinyanga na Tabora wameunda tume ya watu
18 kuchunguza chanzo cha mgogoro wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji wa
wilaya za kishapu mkoani shinyanga na Igunga mkoani Tabora.
Hatua hiyo inafuatia ugomvi wa mipaka uliosababisha vifo vya
watu watano na imeazimiwa katika kamati ya ulinzi na usalama za mikoa hiyo
kilichofanyika katika kijiji cha Magogo ambapo vurugu hizo zimetokea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bwana Ali Lufunga na mkoa wa Tabora Bi Fatuma Mwasa wamesema kikao
hicho kimeazimia kuwa wafugaji walioko katika kijiji cha Magalata wilayani
Kishapu wabakie kwenye eneo lao na wasivuke mto Manonga kulisha Ng’ombe
wao,huku wakulima walioko katika vijiji vya Magogo na IsakaMaliwa wilaya ya
Igunga mkoani Tabora wasivuke Mto Manonga.
Aidha wakulima walioharibiwa makazi katika vijiji vya Magogo na IsakaMaliwa
wametakiwa kuendelea na shughuli zao wakati serikali ikiimarisha ulinzi kwa
kuongeza askari polisi pamoja na kuwatafuta walioharibu makazi yao.
Kwa pamoja wakuu hao wa mikoa wamelaani vitendo vilivyofanywa
na wafugaji wa jamii ya kithatulu na kusema ni vitendo visivyovumilika.
Chanzo:Radio Free Afrika
Post a Comment