MKUTANO WA UWAKILI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WAENDELEA KATIKA KANDA YA KASKAZINI MASHARIKI MWA TANZANIA
Mkutano wa idara ya uwakili ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato unaendelea kwa takribani siku
saba ukihusisha viongozi mbalimbali na washiriki wa makanisa.
Mkutano huo unaoendelea
katika makanisa mbalimbali ya Waadventista Wa Sabato jimbo la kaskazini
mashariki mwa Tanzania[ NETC] ni kwa ajili ya kuwainua washiriki katika kiroho,kuwa na malengo mazuri katika utoaji
pamoja na kujenga uhusiano bora wa ndoa,namna ya kuhusiana kwa karibu na Mungu
lakini pia kuhakikisha uhusiano na jamii unakuwa mzuri.
Akihutubia waumini na wageni walioalikwa
katika kanisa la waadventista wasabato mtaa wa mbauda jijini Arusha mapema wiki
hii mchungaji Julius Mbwambo kutoka chuo kikuu cha Bugema nchini Uganda ameeleza
kuwa uwakili wa mkristo sio tukio la siku moja linalokuja na kupita bali ni
swala endelevu ambalo huwa mtindo wa maisha ya mwanadamu katika kumwakilisha
Mungu Duniani.
Mahudhurio ya mkutano huo katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato mtaa wa Mbauda zaidi ya watu mia mbili kwa siku tangia
ulipoanza siku ya jumamosi mchana.
Post a Comment