MTANGAZAJI

WAGONJWA WASUBIRI HUDUMA ZAIDI YA MASAA 9 HOSPITALI YA MAFINGA

Wagonjwa katika hospitali ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani wa Iringa. wamelazimika kusubiri huduma kwa zaidi ya masaa 9 kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma kwa wakati.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baaadhi ya wagonjwa hospitalini hapo. wamesema kuwa huduma katika hospitali hiyo kwa sasa imekuwa haitolewi kwa wakati kutokana wahudumu wa hospitali hiyo kutopatikana kwa wakati husika hospitalini hapo.


Kwa upande wao akina mama ambao wamefika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya watoto wamelaani vitendo hivyo vya kukaa kwa muda mrefu bila ya huduma hususani katika dirisha la kuchukua dawa.


Aidha Mganga mkuu katika hospitali hiyo Eriki Bakuzi amekanusha kutokuwapo kwa kitendo hicho huku akisema sababu ya kukosekana kwa huduma hiyo ni upungufu rasilimali watu pamoja na miundo mbinu.


Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu pamoja na Mkurugenzi wa wilaya ya mfindi wamefika hospitalini hapo na kushuhudia kuwapo kwa huduma mbovu hospitalini hapo na wamewataka wahudumu hao kufanyakazi kwa kujituma kwa kuwa hospitali hiyo hudumu ina waganga zaidi ya 8 huku wakiwataka watoe huduma kutokana na taaluma yao ikiwa ni pamoja na kufuata misingi ya kazi yao.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.