MTANGAZAJI

WABUNGE WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI WADHAMIRIA KUMUONDOA MADARAKANI SPIKA WA BUNGE

Wabunge wa bunge la jumuia ya Afrika mashariki wamedhamiria kumuondoa madarakani spika wa bunge hilo Bi Magreth Siwa ambaye ni mbunge kutoka Nchini Uganda ambapo april mosi mwaka huu aliahirisha bunge hilo kinyume cha sheria baada ya kugundua kuwa upo mpango unaoendelea kati ya wabunge hao wa kukusanya kura za kumuengua madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha  kwa niaba ya wabunge wa bunge hilo Dr Abdala Mwinyi amesema kuwa wamefuata kanuni na Taratibu zote za kutaka kumtoa spika huyo katika kiti chake kisheria ikiwa ni pamoja na kutimia kwa idadi ya theluthi mbili ya wabunge.


Dr mwinyi amesema kuwa Idadi inayohitajika katika kumng’oa spika wa bunge hilo madarakani ni jumla ya wabunge ishirini na wanne kutoka katika nchi wanachama nasasa idadi hiyo imetimia na kuzidi hadi kufikia idadi ya wabunge thelathini na sita.


Hoja ya kumuondoa madarakani spika huyo iliibuka hata kabla mwenyekiti wa jumuia ya Afrika mashariki Uhuru Kenyata Rais wa Kenya hajalihutubia Bunge hilo marchi ishirini na Tano mwaka huu.


Aidha Tuhuma zinazomkabili spika huyo ni pamoja na kuwadharau wabunge,kuajiri pasipo kufuata Taratibu na sheria,kutowashirikisha wabunge katika kufanya maamuzi ya maswala mbalimbali muhimu yahusuyo bunge hilo na matumizi mabaya na upotoshaji wa Taarifa za bunge.


Wabunge wa bunge hilo wameshaondoka kila mmoja kurudi nchini kwake bila kujua ni lini bunge hilo litaendelea tena na shughuli zake hadi hapo utakapotolewa ufafanuzi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.