MTANGAZAJI

VYETI BANDIA VYA KUKOSA UKIMWI VINAUZWA UGANDA

Imebainika kuwa vyeti bandia vyakukosa ukimwi vinauzwa nchini Uganda.

Shirika la utangazaji la BBC kitengo cha Afrika kimebaini ushahidi wa watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya ukimwi (VVU) yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.


Picha za Filamu zilizochukuliwa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia ambavyo wanavitumia kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata wapenzi wa ngono.


Utafiti ulio fanywa na Mwandishi wa BBC wa Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15, Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hana virusi vya kusababisha ukimwi vya VVU.


Wanaosimamia kliniki hizo walitaka rushwa kati ya Dola 10 na 20 ambazo ni kati ya shilingi za kitanzania laki moja na sitini (16000) na laki tatu na ishirini (320000) kwa kila cheti.


Picha za video zilizopigwa kisiri katika maduka ya kupiga chapa kwenye maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda Kampala zinathibitisha kuwa unaweza kugushi cheti kwa urahisi .


Waziri wa Afya wa Uganda Ruhakana Rugunda amethitibisha kuwa suala hilo ni changamoto kubwa lakini akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashtaki wanaohusika


Chanzo:BBC

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.