MTANGAZAJI

HAKIELIMU YASEMA UGAWAJI WA WALIMU WAPYA NCHINI TANZANIA HAUKUZINGATIA SHULE ZENYE UHABA WA WALIMU

Utafiti uliofanywa na shirika ambalo si la kiserikali la haki elimu unaonyesha kuwa ugawaji wa walimu wapya wa kimkoa haukuzingatia mahitaji yakupunguza uhaba wa walimu katika mikoa husika.

Katika utafiti huo haki elimu imesema mchakato wa ugawaji wa walimu wapya kwa mwaka 2013 na 2014 serikali haikuzingatia shule zenye uhaba wa walimu ambapo wastani wake ni mwalimu 1 kwa wanafunzi 54.


Meneja utafi na uchambuzi wa sera wa haki elimu Godfrey Bonivencha amesema licha ya uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi kitaifa kuboreshwa hadi kufikia mwalimu 1 kwa wanafunzi 40 bado mikoa takribani 12 ya kanda ya magharibi mwa ziwa Victoria haijafikia wastani huo.


Amesema kuwa badala yake mikoa ambayo imevuka lengo la kitaifa Pwana, Dar-es-saalam na Morogoro amabyo imepewa walimu wapya 3733 huku mikoa ya Rukwa,Kigoma na Tabora bado haijafika lengo.


Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa haki Elimu Elizabeti Misokio ameshauri serikali kufanya tathimini itakayoonyesha uwiano unaotakiwa wa walimu pamoja na kuwapa motisha walimu wa shule za pembezoni.


Aidha ameshauri serikali igawe walimu kwa kuzingatia mahitaji kuhamisha walimu kwenye mikoa yenye walimu wengi na kuwapeleka kwenye mikoa yenye uhaba wa walimu na kurejesha hadhi ya waalimu kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.