JAMII YATAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KUCHUNGUZA AFYA
Jamii ya
kitanzania imetakiwa kujenga mazoea na desturi ya kuchunguza afya zao kabla ya
kusubiri kuumwa.
Hayo
yamezungumzwa wakati ambapo Jumla ya madakitari kumi kutoka chama cha
madakitari wanawake Tanzania {Mewata}wakati wa zoezi la kupima afya lililofanyika bure
mapema jana kwa jamii hususani ugonjwa wa saratani ya matiti,kisukari na
shinikizo la damu katika kanisa la waadventista wasabato Njiro.
Akizungumza
na wanahabari Mkurugenzi wa huduma ya afya na kiasi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Njiro Dr. Peter Mabula amesema zoezi limefanikiwa kwa kiwango kikubwa na
zaidi ya wanawake mia moja wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti,kisukari
na shinikizo la damu kati yao wachache wameonekana na viashiria vya magonjwa
hayo hivyo idara ya afya na kiasi ya kanisa kwa kushirikiana na chama cha madakitari
wanawake{ MEWATA}pamoja na wadau wengine wa afya wanafanya mpango wa kuwapatia
huduma ya matibabu wale wote walioonekana na viashiria hivyo.
Hata hivyo wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo muhimu wameipongeza
idara ya afya na kiasi ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Njiro, kwa kuratibu
na kuandaa mpango huo ambao wameuita ni msaada wa karibu kwa jamii ya mwanamke
Mtanzania. hivyo wameomba elimu itolewe pia kwa wanaume kujua na kutambua kuwa,
hata wao wanaweza kupatikana na ugonjwa wa saratani ya matii, hivyo wajitokeze
kuchunguza afya zao ili kupatiwa huduma mapema.
Na Abel Kinyongo
Post a Comment