MTANGAZAJI

NKUTANO WA WAFANYAKAZI WA TAASISI ZA UNIONI MISHENI YA KUSINI WAENDELEA MOROGOROMkutano wa wafanyakazi wa wataasisi mbalimbali za Kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni Misheni ya kusini mwa Tanzania umeingia siku ya pili,huku msisitizo mkuu ukiwa katika kipengele cha kukumbushana.

Mhazini mkuu wa Unioni Misheni  ya Kusini mwa Tanzania
Bw.Jack Manongi amesema kuwa  mambo matatu muhimu ambayo ni yanayotazamwa ni maswala ya bima kwa wafanyakazi,utunzaji wa fedha na matumizi ya fedha.Akifafanua swala la bima amedai kuwa ni swala nyeti kwa wafanyakazi na taasisi zote zinaagizwa kuhakikisha zinazingatia  haki ya kila mfanyakazi kuwa na bima iliyohuishwa.

Akizungumzia uwasilishwaji wa fedha katika mifuko ya hifadhi ya jamii Bw.Manongi ameeleza kuwa,ni kosa kwa taasisi kuchelewesha michango mbalimbali ya wafanyakazi katika mifuko ya jamii kwakuwa jambo hilo hupelekea taasisi kutumbukia katika tatizo la madeni.

Mkutano wa wafanyakazi wa Taasisi za huduma ya nyumbani na elimu (HHES) Sauti ya unabii vyombo vya Habari (VOP/TAMC) na taasisi ya uchapishaji (TAP) umefunguliwa jana na M/kiti wa Union mission ya kusini mwa Tanzania Mch.Magulilo MWakalonge.

Na Manase Rusaka-Morogoro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.